Na , Geofrey A.Kazaula
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Generali Marco E. Gaguti amewatia moyo watoto wa Shule ya Msingi Kitengule na kuwataka kutokata tama kwani Serikali ipo kwa ajili yao.
Akiwa Shuleni hapo, katika mwendelezo wa ziara yake Wilayani Karagwe, Kiongozi ametumia muda wake kuwasikiliza wanafunzi na hasa wale wenye mahitaji maalum.
Kiongozi huyo alianza kwa kutaka kujua ndoto za kila mmoja na watoto walieleza kile wanachokiona ni muhimu kwao kwa siku za badae huku wengine wakimwambia juu ya ndoto zao za kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanza nia kwa siku za usoni.
Mkuu huyo wa Mkoa aliwasikiliza wanafunzi na kisha alianza kuwasihi kusoma kwa bidii na malengo ili waweze kufikia ndoto zao.
‘‘ Tumieni muda wenu kusoma kwa bidii ili mfikie ndoto zenu kwani Serikali ipo kwaajili yenu, mimi kama Mkuu wenu wa Mkoa nimeona nifike kuongea nanyi ili mkae mkijua kabisa kuwa Serikali hii inawajali na hasa watoto kama nyie wenye mahitaji maalum’’ alisema kiongozi huyo.
Aidha aliwakabidhi mbuzi wawili ili waweze kujipatia kitoweo na kusisitiza kuwa Serikali ina wajali na kamwe wasijisikie upweke.
Kiongozi huyo alisisitiza kuwa Serikali kwa kushirikiana na uongozi wa Shule itahakikisha changamoto zilizopo Shuleni hapo zinapatiwa ufumbuzi na kuweka mazingira rafiki kwa kwa watoto hao ili waweze kujisomea.
Kwaupande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kitengule Ndg, Raymond Emanuel alimpongeza Mh, Mkuu wa Mkoa kwa kuamua kuitembelea shule hiyo na hasa kuwatia moyo wanafunzi.
‘‘Nampongeza sana Mkuu wetu wa Mkoa kwa kufika na kuwatia moyo watoto wetu kwani kwa kufanya hivi wanaona kabisa kuwa Serikali iko upande wao’’. alieleza Mwalimu huyo
Ziara ya Siku moja ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Generali Marco E. Gaguti Wilayani Karagwe ilihitimishwa kwa Mkuu huyo wa Mkoa kfanya ukaguzi wa miradi mbalimbali,kufanya mikutano ya hadhara pamoja na kusikiliza na kutatua kero za wananchi.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.