Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania Yatambulishwa Wilayani Karagwe
Na Innocent E. Mwalo, KARAGWE
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Jumanne ya tarehe 19/09/2017 ilipata nafasi ya kutambulishwa Wilayani Karagwe kupitia kikao cha Timu ya Wataalam (CMT) kilikuwa kinafanyika siku hiyo.
Mapema wataalam toka Benki hiyo waliwasili sehemu kilipokuwa kinafanyikia kikao hicho wakiwa wameongozana na Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Mh. Innocent Nsena na kisha wakapata nafasi kutoka kwa Mwenyekiti wa Kikao, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Karagwe, ndugu Godwin M. Kitonka ya kujitambulisha.
Mkuu wa Msafara, Geofrey Mtawa aliwatambulisha wataalam wengine alioambatana nao na kisha kutoa maelezo kuhusu uanziswaji wa Benki hiyo.
Mtawa aliwaeleza wajumbe kwamba Benki ya wakulima ilizinduliwa Agosti 08, 2015 ambapo ilianzishwa kwa madhumuni makubwa mawili ambayo ni kusaidia upatikanaji wa utoshelezi na usalama wa chakula ambao ni endelevu nchini Tanzania na kusaidia kuchagiza Mapinduzi ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda kilimo cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umasikini.
Mtawa alikiambia kikao hicho kwamba kwa sasa Benki hiyo inafanya kazi katika kanda nane hapa nchini Tanzania na mkoa wa Kagera utakuwa ni mmoja wa mikoa nane latika Kanda ya Ziwa ambapo ofisi zake zinatarajiwa kujengwa jijini Mwanza ambapo ofisi hizi za kanda zinatajiwa kufanya kazi na mikoa na wilaya na huku kwenye Halmashauri mdau wa kuwaunganishi wakulima akiwa Halmashauri ya wilaya kupitia kwa Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika.
Mtawa aligusia baadhi ya malengo ya kimkakati ya Benki hiyo kuwa ni kuinua uzalishaji wenye tija katika sekta ya Kilimo kwa kuendeleza miundombinu muhimu, mathalani skimu za umwagiliaji, usafirishaji, hifadhi ya mazao, usindikaji na masoko.
Lengo jingine ni kuwa Benki kiongozi ya maendeleo ya kilimo pamoja na kuhamasisha mabenki mengine na taasisi nyingine za kifedha kutoa fedha kwenye mnyororo mzima wa Kilimo.
Baada ya utambulisho wa Benki hiyo kikao cha Timu ya Menejimenti kiliendelea huku kikiweka mikakati kadhaa katika suala nzima la ukusanyaji wa mapato ya Halmasahuri.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.