Sunday 22nd, December 2024
@Some vilage of Karagwe District Council
Mpango wa Tatu, Sehemu ya Pili ya Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini, (TASAF), uliozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli, Julai 17,2020, dirisha la tatu la Mradi wa TASAF sehemu ya pili unatajiwa kufanyika kwa takribani siku kumi, kuanzia Februari 10, 2021 wilaya Karagwe ambapo jumla ya shillingi 444,864,000 zitahawilishwa kwa wanufaika wapatao 8,195 katika dirisha la tatu la mradi huo.
Evodius Rwangoga, Mratibu wa Mradi wa TASAF wilayani hapa amebainisha kwamba mradi huu wa TASAF Awamu ya Tatu, Sehemu ya Pili ni wa tofauti na kidogo na ile ilitekelezwa katika Awamu za Kwanza na za Pili kutokana na ukweli kwamba utekelezaji wa Awamu ya Tatu sehemu ya Pili umejikita na kusisitizwa kwa walengwa kuwekeza katika miradi midogomigo na ya kati ili iweze kuwasaidia kujipatia mahitaji yao muhimu.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.