Sunday 22nd, December 2024
@Karagwe
Geofrey A.Kazaula
Maandalizi ya kuupokea Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2019 Katika Wilaya ya Karagwe yanaendelea ambapo kwa ujumla, Mwenge wa Uhuru Utakuwa katika Mkoa Wa Kagera mnamo mwezi wan ne ( 4) 2019
Inakadiliwa kuwa kwa Wilaya ya Karagwe, mwenge wa uhuru utaingia kuanzia tarehe 25/04/2019
Ukiwa Wilayani Karagwe, Mwenge wa Uhuru utatembelea na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo kama ifuatavyo:-
Kikundi cha watu wenye Ulemavu ( Tumaini Nyaishozi), Ujenzi wa Kituo cha Afya Nyakayanja, Klabu ya wapinga Rushwa Shule ya Sekondari Nyakahanga, Ujenzi wa barabara kwa kiwango cha Lami Mjini Kayanga na Omurushaka , Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Karagwe, Ujenzi wa mabweni na vyumba vya madarasa katika chuo cha Ufundi KDVTC , Kikundi cha Vijana ( Lemon Villa) , Kikundi cha wanawake Juhudi na Maarifa na maonesho mabanda ya UKIMWI, Malaria na mabanda ya wapinga Rushwa.
Hata hivyo, mwenge wa uhuru utalala katika uwanja wa changarawe Kayanga na wananchi wote mnakaribishwa kushiriki kikamilifu.
Katika uwanja huo kutakuwa na matukio mbalimbali kama burudani pamoja na ushuhuda mbalimbali wa watu wanao ishi na ugonjwa wa UKIMWI. Pia kutakuwa na huduma mbalibali kama upimaji wa UKIMWI kwa hiari pamoja na upimaji wa ugonjwa wa Maralia.
Taarifa zaidi zitaendelea kutolewa na Maafisa Habari kupitia Kitengo cha TEHAMA kadili maandalizi yanavyo endelea.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.