Sunday 22nd, December 2024
@Karagwe
MWENGE WA UHURU WILAYANI KARAGWE , 2017
Na, Geofrey A.Kazaula
Maandalizi ya kuupokea Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2017 Katika Wilaya ya Karagwe yanaendelea ambapo kwa ujumla, Mwenge wa Uhuru Utakuwa katika Mkoa Wa Kagera kuanzia tarehe 1/08/2017 hadi tarehe 08/08/2017.
Wilaya ya Karagwe inatarajia kuupokea Mwenge wa Uhuru mnamo tarehe 03/08/2017 ambapo mwenge huo utakuwa unatokea Wilaya ya Ngara.
Ukiwa Wilayani Karagwe, Mwenge wa Uhuru utatembelea na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo kama ifuatavyo:-
Shamba la miti Katika kata ya Rugu kijiji cha Misha ,Club ya wapinga Rushwa katika Shule ya Sekondari Nyakahanga – Kata Nyakahanga ,Kiwanda cha kukamua mafuta ya Arizeti cha Dr Marco Bitesigirwe kilichopo Kata ya Nyakahanga.
Miradi mingineitakayo tembelewa ni pamoja na Mabweni mawili ya Wavulana katika Shule ya Sekondari Bugene, Kata Bugene , Kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa mradi wa maji mjini kijiji cha Rukajange eneo la Kishao Kata ya Bugene ,Mradi wa Vijana – Fundi seremala mjini Kayanga , Kata ya Kayanga .
Aidha, Mwenge wa uhuru utatembelea na na kuweka Jiwe la Msingi katika ujenzi wa wodi ya wanaume katika kituo cha Afya Kayanga pamoja na ujenzi wa Chumba cha Kuhifadhia maiti katika Kituo cha Afya Kayanga kata Kayanga,Kutembelea banda la wanawake wajasiriamali wa kikundi cha MVIKAKAKI katika uwanja wa mkesha Kayanga na Kutembelea banda la TAKUKURU katika uwanja wa mkesha . Kayanga.
Katika uwanja huo kutakuwa na matukio mbalimbali kama burudani pamoja na ushuhuda mbalimbali wa watu wanao ishi na ugonjwa wa UKIMWI. Pia kutakuwa na huduma mbalibali kama upimaji wa UKIMWI kwa hiari pamoja na upimaji wa ugonjwa wa Maralia.
Taarifa zaidi zitaendelea kutolewa na Maafisa Habari kupitia Kitengo cha TEHAMA kadili maandalizi yanavyo endelea.
Wananchi wote mnakaribishwa kushiriki kuupokea mwenge wa uhuru wilayani Karagwe ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘’ Shiriki kukuza Uchumi wa Viwanda kwa maendeleo ya nchi yetu’
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.