Sunday 22nd, December 2024
@Karagwe District Council
Kikao cha Baraza la Madiwani, ajili ya kujadili na kupitisha mapendekezo ya Bajeti kwaya Halmashauri ya Wilaya kwa mwaka wa Fedha 2021/2022 kinatarajia kufanyika kwa muda siku mbili kuanzia Machi 09- 10/2021 katika Ukumbi wa Vijana Rafiki wa Angaza. Kikao ni kikao cha kwanza cha Bajeti tangu kuchaguliwa kwa Baraza jipya mnamo Novemba 2020, kimeazimia kwa kauli moja kuongezwaa kikao hiki pamoja na mambo mengine kinatajiwa kujadili na kuptisha mipango mbalimbali iliyobuniwa na Halmashauri ya wilaya kwa minajili ya kuongeza ukusanyaji wa mapato.
Aidha katika kikao hiki wenyeviti wa Kamati tatu za kudumu za Halmashauri ya Wilaya yaani; Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango chini ya Mwenyekiti wake Mh. Wallace Mashanda, Kamati ya Elimu, Afya na Maji chini ya uenyekiti wa Mh. Charles Beichumila, na ile ya Ujenzi, Uchumi na Mazingira inayoongozwa na Mh. Valence Kasumuni wanatarajia kuwasilisha kwa Baraza hili taarifa juu ya mapendekeo ya mpango na Bajeti kwa mwaka wa fedha 2021/2022 kama yalivyopitishwa na wajumbe wa kamati hizo. Katika kikao hicho taarifa zote kuhusu mapato na matumizi ya Idara/Vitengo vya Halmashauri ya Wilaya zitawasilishwa kwenye kikao hicho.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.