Ujenzi wa Miundo Mbinu ya Kituo cha Afya Kayanga Wapamba Moto.
Na Innocent E.Mwalo, KARAGWE.
Ujenzi wa Miundombinu ya Kituo cha Afya cha Kayanga ambacho ndio kituo kikubwa cha Afya Wilayani hapa chenye uwezo wa kuhudumia wananchi takribani 2,400 mpaka 3,500 kwa mwezi unaendelea kwa kasi kubwa.
Katika ukaguzi uliofanywa na Mwandishi wa habari hii imebainika kwamba kwa sasa ujenzi wa miundo mbinu katika kituo hiki unakwenda kwa kasi kubwa huku huduma ya upasuaji iliyoanza kutolewa tarehe 08/12/2016 katika kituo hiki ikiimarika zaidi ya mara dufu ambapo idadi ya wanawake wanaojifungulia katika kituo hiki imeongezeka kutoka wanawake 40 na 45 ambao walikuwa wanajifungulia kwenye kituo hicho hapo awali hadi kufikia wanawake 110 na 140 kwa mwezi huku vifo vya akina mama vikipungua kutoka kutoka vifo 15 hadi vifo 05 ambayo ni sawa na asilimia 69.
Ujenzi wa miundo mbinu unaoendelea katika kituo hiki cha afya hiki unalenga kutibu changamoto zilizoonekana hapo hapo katika eneo hilo lakini pia athali za tetemeko la ardhi lililotokea katika mkoa wa Kagera mnamo 10/09/2016 na kusababisha changamoto kadhaa ikiwemo kuharibika kwa miundombinu ya kituo hiki cha afya na makazi ya watu.
Kufuatia athari hizo za tetemiko la ardhi, Kituo hiki cha afya kilipokea kiasi cha Tsh.170,714,452.18 mnamo 16/06/2017 kutoka Mfuko wa Maafa wa Mkoa kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya wazazi, chumba cha kuhifadhia maiti na power house ambapo kwa mujibu wa Mganga Mkuu wa Wilaya Karagwe, Dkt. Libamba Sobo fedha hizo ziliweza kupelekwa moja kwa moja katika kituo hiki cha afya kwa ajili ya kutekeleza mradi huo kwa kutumia utaratibu wa “Force Account”
Aidha kutokana na ahadi iliyotolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Mh. Jenista Mhagama (Mb) aliyoitoa mnamo 11 -13 /07/2017 wilayani hapa na mkoani Kagera kwa ujumla, kituo cha Afya cha Kayanga kimeweza kupokea takribani kiasi cha 72,989,530 ikiwa ni kutekeleza ahadi yake hiyo juu ya urejeshwaji wa miundombinu hiyo kwenye kituo cha Afya cha Kayanga.
“Sio hivyo, Halmashauri ya Wilaya Karagwe imeweza kupokea pia kiasi cha Tsh. 500,000,000 kutoka Serikali kuu chini ya mradi wa kuboresha vituo vya afya ikiwa ni kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa majengo wa Kituo cha Afya cha Kayanga kwa ufadhili wa Serikali ya Canada”, alisema Dkt. Sobo.
Aidha Dkt. Sobo aliendelea kusisitiza kwamba tayari kuna vifaa vya ujenzi vilivyopokelewa kutoka ghala la maafa mkoa ni pamoja na mabati ya kuezekea 280, matofali ya block 8,600, wire Pv 2.5 mita 400 na wire pv 1.5 mita 500.
Kutokana na michango hiyo tayari tayari ujenzi wa mradi wa wodi ya wazazi, chumba cha kuhifadhia maiti na power house ambapo ujenzi wake umekamilika kwa zaidi ya asilimia 92.3
Aidha ujenzi wa majengo mengine ambayo ni wodi ya akina mama, nyumba ya mtumishi, jengo la huduma za wagonjwa za afya ya uzazi na mtoto pamoja nahuduma za wagonjwa wa nje (OPD na RCH) na jengo la wodi ya wanawake umekamilika kwa asilimia 89.02.
Itakumbukwa kwamba hapo awali kituo kilipokea Tshs. 743,704,057.20 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo, ambapo fedha zilizokwisha kutumika ni Tsh.591,688,477.00 na zilizobaki ni Tsh. 152,015,580.20 ambazo zinaendelea kutumika ili kukamilisha ujenzi na ukarabati wa majengo yanayokusudiwa ambayo ni wodi ya wagonjwa, jengo la upasuaji, jengo la utawala, store ya dawa na jengo la CTC ambapo ujenzi wake unatajiwa kuanza mwezi huu.
Kituo hiki cha Afya Kayanga ni kituo pekee cha Afya kilichopo ndani ya Wilaya Karagwe ambacho kilianza kutoa huduma mwaka 1961 ambapo kilipoanza muda huo ilikuwa kama sehemu tu ya kutolea huduma ya kwanza (Health post) ambapo baadae kulipandishwa hadhi na kuwa kituo cha Afya.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.