MASHIRIKA YASIYOKUWA YAKISERIKALI KARAGWE DC YAASWA KUDUMISHA USHIRIKIANO ENDELEVU NA SERIKALI ILI KULETA MATOKEO CHANYA KWA WANANCHI.
Mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) yanayofanya shughuli zake Katika Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe yameaswa kudumisha ushirikiano endelevu na Serikali ili yaweze kuleta matokeo chanya kwa Wananchi ikiwemo uboreshwaji wa huduma za afya, mafunzo ya kilimo bora kwa jamii, upatikanaji wa maji safi pamoja na uwezeshwaji wa kiuchumi kwa wananchi kupitia mikopo ya wajasiriamali.
Wito huo umetolewa tarehe 27/06/2025 wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa jukwaa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) kwa ngazi ya Halmashauri uliofanyika katika ukumbi wa SAWAKA Wilayani Karagwe ambapo Mashirika haya yaliwasilisha taarifa za utekelezaji wa shughuli zao kwa mwaka 2020 hadi 2025.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe Bi.Henrietta William ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya jamii amasema kuwa Mashirika yasiyo ya kiserikali yanawajibu wa kushirikiana bega kwa bega na Serikali kupitia Halmashauri katika utendaji kazi wake ili kuepuka migongano isiyo ya lazima na Serikali hususani kwenye ulipaji kodi mbalimbali na uwasilishaji wa taarifa sahihi za utekelezaji wa majukumu yao.
Aidha, kwa kipindi cha miaka mitano (2020 - 2025) Jumla ya Mashirika 32 yasiyo ya kiserikali yaliyosajiliwa kufanya shughuli zake katika Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe kwa mchanganuo ufuatao Mashirika ya ndani 6, Mashirika ya Kitaifa 25 na Mashirika ya Kimataifa 1 kwa miaka yote hiyo kiasi cha shillingi 6,538,874.59 kimetumika katika utekelezaji wa miradi mbalimbali.
Hatahivyo, Kikao hiko kililenga kufanya tathimini ya utekelezaji wa Mashirika hayo kwa miaka 5 mfululizo kwa kufuata kauli mbiu isemayo "Tathmini ya mchango wa Mashirika yasiyo ya kiserikali katika Maendeleo ya Taifa 2020/2021 - 2024/2025 Mafanikio, Changamoto, Fursa na Matarajio ".
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.