Wadau wanaotoa huduma za afya (sekta binafsi ) na umma wamekutana na kujadiliana namna ya kuendelea kuimarisha huduma za afya katika Halmashauri ya wilaya ya Karagwe. Kikao hicho kimefanyika Agosti 1, 2022 katika ukumbi wa ELCT-Karagwe.
Mwenyekiti wa kikao hicho alikuwa Mkuu wa wilaya ya Karagwe, Mhe. Mwl. Julieth Binyura ambaye aliwaagiza waratibu wa ubia na ushirikiano kati ya sekta binafsi na umma kuwa na vikao vya mara kwa mara kwani vitasaidia kutatua matatizo ya kiafya kwa wananchi wa Karagwe.
Aidha, Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Karagwe, Mhe. Wallace Mashanda alishauri kuwa mikataba ya ubia na ushirikiano iwekwe wazi ili wajumbe waipitie na kushauri ipasavyo kwa maslahi ya kuwalinda wanchi.
Naye Dkt. Kawia Hassan kutoka ofisi ya mganga Mkuu wa mkoa wa Kagera alibainisha kuwa watoa huduma za afya katika maeneo ambayo serikali haijafanikiwa kuwa vituo vya kutolea huduma wamekuwa wanasaidia sana.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.