Na Geofrey A.Kazaula
Serikali ya awamu ya tano chini ya Mh, Rais Dr . John Pombe Magufuli imetoa jumla ya Shilingi Billioni moja nanusu kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Karagwe.
Ujenzi huo tayari umeanza kwa awamu ya kwanza na majengo saba ambayo ni pamoja na Jengo la Utawala, Jengo la wagonjwa wan je (OPD ), Jengo la X-ray , Jengo la maabara, Jengo la wodi ya akina mama, Jengo la stoo ya dawa na Jengo la Kufulia.
Hadi sasa ujenzi huo unaendelea vizuri kwa kutumia mfumo wa ‘‘Force Account ’’ inayo wajumuisha mafundi wa ndani.
Akizungumza na watumishi wanaosimamia ujenzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe Ndg, Godwin M.Kitonka amesisitiza juu ya kufanya kazi kwa ufanisi na kusimamia kila hatua ya ujenzi huo.
‘‘ Nitoe wito kwenu mnaosimamia vifaa pamoja na ujenzi mfanye kazi kwa uadilifu wa hali ya juu kama mlivyosimamia miradi iliyotangulia ya ujenzi wa Vituo vya Afya hadi ika kamilika bila matatizo na mimi ntakuwa najiridhisha kila siku hadi kukamilika kwa mradi huu’’. Amesema Kiongozi huyo.
Kwaupande wake msimamizi Mkuu wa ujenzi huo Eng, Magai Kakuru amefafanua kuwa majengo hayo saba yanayojengwa yatasimamiwa kwa ukamilifu na kuhakikisha yanakamilika kulingana na mkataba unavyotaka ambapo hadi mwishoni mwa mwezi Aprili 2019 majengo hayo yatakuwa yamekamilika.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.