Mkurugenzi wa Uchaguzi Ndugu Ramadhani Kailima amewataka Maafisa Habari wa Serikali kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya Kwanza zoezi linalotarajiwa kuanza Julai 1, 2024
Kauli hiyo imetolewa Juni 15, 2024 wakati wa Mkutano wa Tume na Maafisa Habari wa Mikoa na Halmashauri uliofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam
"Ndugu Maafisa Habari, uboreshaji huu unahusu kila mwananchi mwenye sifa, Tumieni njia mbalimbali kuelimisha jamii umuhimu wa kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga awamu ya kwanza" Ndugu Ramadhani Kailima.
Awali akiwasilisha mada kuhusu uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Awamu ya Kwanza, Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura Bi. Giveness Aswile amesema zoezi hilo linatarajia kuanza Julai 01, 2024 na baada ya uboreshaji inatarajiwa kuwa Daftari litakuwa na jumla ya wapiga kura 34,746,638.
“Katika uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa kuzingatia matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022, Daftari linatarajiwa kuwa na wapiga kura 34,746,638 kutoka 29,754,699 ya mwaka 2020 hili ni ongezeko la wapiga kura wapya 5,586,433 sawa na asilimia 18.7,” amesema Bi. Givennes
Ameongeza kuwa katika zoezi hilo wapiga kura 4,369,531 wanatarajiwa kuboresha taarifa zao na wapiga kura 594,494 wataondolewa katika Daftari kwa kupoteza sifa za kuwa wapiga kura.
Akizungumzia kuhusu mfumo mpya saidizi unaofahamika kama Online Voters Registration System, (OVRS) amesema mfumo huu utawawezesha wapiga kura walioandikishwa kuanzisha mchakato wa uboreshaji kwa njia ya mtandao kupitia simu ya mkononi au Kompyuta kubadilisha taarifa au kuhama jimbo au kata au kubadilisha na kuhama.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.