Halmashauri ya wilaya ya karagwe imeanza maandalizi kwa ajili ya kuhakikisha zoezi zima la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura linaenda vizuri.Afisa Mwandikishaji wa Wilaya akishirikiana na Maafisa Tehama pamoja na Maafisa Wandikishaji wasaidizi ngazi ya Wilaya wamehakikisha kuwa mafunzo kwa watendaji wa Kata kuhusiana na shughuli nzima ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga Kura linaendeshwa kwa kuzingatia sheria na taratibu.
Mafuzo hayo yamefanyika siku mbili kuanzia tarehe 25-26/09/2019 katika ukumbi wa Angaza mjini kayanga.Watendaji wote wa kata 23 wamepatiwa mafunzo na wapo tayari kwa zoezi zima la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga Kura. Pia wanatarajia kuwa na mafunzo ya BVR Kit Operators na waandikishaji wasaidizi wa vituo vya kuandikishia wapiga kura kuanzia tarehe 29-30/09/2019.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.