KAMATI YA LISHE YAKETI KUJADILI UTEKELEZAJI WA AFUA ZA LISHE, KIPINDI CHA ROBO YA TATU 2024/2025.
Kamati ya Lishe Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe leo Aprili 22, 2025 imefanya Kikao cha kawaida cha Kujadili taarifa za utekelezaji wa afua za lishe kwa kipindi cha Robo ya Tatu kuanzia mwezi Januari hadi Machi 2025.
Akifungua kikao hicho kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Dr. Agness A. Mwaifuge amesema kuwa kikao hichi ni muhimu sana kwani Halmashauri yetu inaendelea kutekeleza maagizo ya upatikanaji wa lishe kwa vitendo, Serikali ya awamu ya sita imeendelea kulipa umuhimu wa kipekee suala la lishe bora katika jamii.
Kwa upande wake Afisa Lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe Bi; Asnath Thobias amesema kuwa Divisheni ya Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii imeendelea kutekeleza afua za Lishe na kufanikiwa kutoa elimu kwa Wananchi kupitia vikao mbalimbali kuhusu masuala ya lishe bora na ulaji wa mlo kamili hasa kupitia mazao yetu tunayolima.
" Katika kipindi cha robo ya tatu, tumefanikiwa kutekeleza afua za lishe kwa kutumia kadi alama, ambapo tumepima viashiria mbalimbali ikiwemo kiashiria cha upimaji wa utapiamlo, kiashiria cha utoaji wa chakula Shuleni angalau mlo mmoja, kiashiria cha usimamizi shirikishi na kwa hili tumefanikiwa sana kama kadi alama inavyoonesha". Alisema.
Sambamba na hilo Idara mbalimbali ziliwasiliisha taarifa za utekelezaji wa Afua za lishe kwa kipindi cha robo ya tatu ikiwemo idara ya Elimu ya Awali na Msingi, Idara ya Elimu Sekondari, Idara ya Maendeleo ya Jamii, Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, TASAF pamoja na mashirika binafsi ikiwemo Redio Karagwe, Redio Fadeco, CBIDO, RUWASA na Humuliza pamoja na mashirika ya Dini ya Kiislamu na Kikristo.
Aidha, katika kikao hicho wajumbe walitoa ushauri juu ya masuala ya Lishe bora na kuzingatia usafi pamoja na kukubaliana kuendelea kutoa hamasa na elimu kwa wananchi juu ya masuala ya lishe ili kuendelea kuboresha hali ya lishe na kupitia mabonanza mbalimbali yaendelee kutoa elimu ya lishe ili kila mwananchi apate elimu hiyo itakayosaidia kuondoka na suala la lishe duni na utapiamlo.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.