NA Frank I. Ruhinda
Hatimae zoezi lilokuwa likiendeshwa hapa wilayani Karagwe takilibani kwa kipindi cha mwezi mzima la uelimishaji kuhusu ukatazaji wa mifuko ya plastiki linaelekea mwaisho kwa mafanikio makubwa japo chaangamoto ndogondogo haziwezi kukosekana.
Hayo yalielezwa na mwenyekiti wa timu ya wilaya ambaye ni mkurugenzi mtendaji Godwini M Kitonka kuwa uelimishaji huo ulifanyika kwa kutuia vyombo vya habari vya kijamii vilivyoko hapa kama vile FADECO radio na KARAGWE FM.
Hata hivyo zoezi hili ninafanyika kwenye magulio siku tofauti kama kama vile hapa Kayanga Omurusha lakini pia kwenye minada ya mifugo kama vile Nyaishozi na Ihanda.
Alisema hadi kufikia leo hii tayari mifuko ambayo inapendekezwa kutumika imeishatapakaa kila sehemu na ile ya parastiki tayari wananchi wenyewe wenye uwezo wateketaza wenyewe la sivyo wengine wanaonyeshwa sehemu maalumu za kukusanywa na badae kuteketezwa.
Baada ya walaka kutoka kuhusu kuundwa kwa timu ya kuteketeza mifuko ya plasitiki ilipewa ufafanuzi kuhusu zoezi hili si la kutumia nguvu ni kutoa elimu kwanza na kuona mwitikio jaamii ambacho ndocho kitu kilifanyika bado kinaendelea hadi sasa.
Zoezi hili linaenda sambamba na sera ya taifa ya usafi wa mazingira ambapo na upandaji miti pamoja na kuandaa maeneo malumu ya kuweka madampo siyo kuyaweka katikati ya makazi ya watu na katikati ya masoko.
Hata hivyo zoezi hili limeeleweka kilahisi kwani hadi sasa mifuko hiyo haionekani mtaani kama ilivyokuwa imezoeleka.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.