Mkuu wa wilaya ya Karagwe Mhe: Julius Kalanga Laizer, amewataka wananchi kuacha kupuuza huduma mbalimbali za chanjo zinazotolewa na serikali kwa watoto, kwani zimethibitishwa na wataalamu wa afya
Hayo yamesemwa na mkuu wa Wilaya ya Karagwe Julius Laizer, wakati akizindua kampeni ya chanjo ya matone ya vitamini A kwa watoto wenye umri wa miezi sita hadi mika 5 iliyozinduliwa katika kituo cha Afya Kayanga ikielezwa kuwa zoezi hilo litaendelea mpaka tarehe 30 mwezi huu.
“Chanjo zinazotolewa na serikali ni salama hivyo wananchi wasisite kuwapeleka watoto wao kupata chnjo hiyo kwani ni salama na haina madhara yoyote”
Aidha, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe Henirietha William ambaye pia ni Afisa maendeleo ya jamii Wilaya ya Karagwe kabla ya uzinduzi amesema kwenye kampeni hii kutakuwa na utoaji wa matone kwa watoto wa miezi sita hadi miezi 59 yaani miaka mitano pamoja na utoaji wa dawa za kutibu minyoo kwa watoto wenye umri wa mwaka mmoja hadi miaka 5 sambamba na upimaji wa hali ya lishe kwa watoto hao.
Pia, Afisa lishe Wilaya ya Karagwe, Lustika Mgumba, amesema lengo la kufanya kampeni hii ni ili kusaidia watoto kuimarisha kinga ya mwili na kuzuia magonjwa mbalimbali yakiwemo ya kuhara na kupelekea mkoa kuendelea kuondoza kwa udumavu na utapiamlo.
Kampain ya chanjo hiyo hutolewa mala mbili kwa mwaka mwezi wa sita na mwezi wa 12 na Kauli mbiu ya kampaini ya Chanjo ya matone ya vitamini A, ni “HUDUMA ZA MWEZI WA AFYA NA LISHE YA MTOTO NI MUHIMU KWA UKUAJI WA MAENDELEO YA MTOTO TUMFIKIE KILA MTOTO MAHALI POPOTE ALIPO”.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.