ELIMU YA MSINGI.
Mwaka 2015 Wilaya ina jumla ya Shule za Msingi 117 zikiwemo za serikali 110, zisizo za serikali 7.
UANDIKISHAJI WA DARASA LA KWANZA.
Mwaka 2015 Wilaya imeweza kuandikisha jumla ya wanafunzi 6,663 (asilimia 92), wavulana 3,366 na wasichana 3,297 kati ya wanafunzi 7,246 waliotarajiwa kuandikishwa.
IDADI YA WANAFUNZI.
Hadi kufikia Juni mwaka 2016, Wilaya ya Karagwe ina jumla ya wanafunzi 61,223, wavulana 29,865 na wasichana 21,358 na kwa shule zisizo za serikali zina wanafunzi wavulana 636 na wasichana 611, jumla 1,247. Kwa ujumla wa shule za serikali na zisizo za serikali zina wavulana 30,501 na wasichana 31,969, jumla kuu 62,470.
IDADI YA WALIMU.
Wilaya ina jumla ya walimu 1,396 wa kike 601 na wa kiume 795. Hii ni sawa na uwiano wa 1:44 yaani mwalimu 1 kwa wanafunzi 44. Hata hivyo bado upo upungufu wa walimu 379 hii ni kutokana na wingi wa wanafunzi wanaosajiliwa kuingia darasa la kwanza na baadhi ya walimu kustaafu.
MIUNDO MBINU.
Hali ya miundo mbinu katika Shule za Msingi ni kama inavyoonyeshwa kwenye jedwali hapo chini.
Jedwali Namba 3 (Miundo mbinu ya shule za msingi kwa mwaka 2016)
Na. |
Aina |
Mahitaji |
Yaliyopo |
% |
Upungufu |
% |
1. |
Vyumba vya madarasa
|
1,829 |
888 |
49 |
941 |
51 |
2. |
Nyumba za walimu
|
1,829 |
334 |
19 |
1,495 |
81 |
3. |
Vyoo (wavulana) matundu
|
2,144 |
6,886 |
32 |
1,458 |
68 |
4. |
Vyoo (wasichana) matundu
|
2,144 |
684 |
32 |
1,460 |
68 |
5. |
Ofisi za walimu wakuu
|
107 |
93 |
87 |
14 |
13 |
6. |
Ofisi za walimu
|
121 |
80 |
66 |
41 |
34 |
7. |
Madawati
|
29,446 |
19,647 |
67 |
9,799 |
33 |
8. |
Viti
|
3,341 |
1,691 |
51 |
1,650 |
49 |
9. |
Meza
|
3,034 |
1,326 |
44 |
1,708 |
56 |
10. |
Matenki ya maji
|
134 |
69 |
51 |
65 |
49 |
VITABU.
Hadi Mwezi Februari, 2016 uwiano wa kitabu kwa wanafunzi umefikia 1:5. Hii ni baada ya kuanza kupokea vitabu vilivyonunuliwa na Serikali (Capitation) na Shirika lisilo la kiserikali la TWAWEZA na vitabu vya chenji ya Rada na wadau wengine.
VYUO VYA UFUNDI.
Wilaya ina Vyuo vya Ufundi 3 hadi kufikia mwaka huu 2016. Chuo kimoja ni cha Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe (KDVTC), Chuo 1 ni cha mtu binafsi (KVTC) na Chuo 1 ni cha Kanisa la Kilutheri Tanzania (Lukajange ELCT).Vyuo hivi vinatoa elimu ya kuwawezesha vijana waweze kujitegemea na kujiajiri katika fani mbali mbali.
ELIMU YA SEKONDARI
IDADI YA SHULE KATIKA WILAYA
Wilaya ina jumla ya shule za Sekondari 25 zenye jumla ya wanafunzi 9,064 kati yao 4,330 wakiwa ni wavulana na 4,734 wasichana. Jedwali lifuatalo linaonesha idadi ya shule na wanafunzi waliosajiliwa katika shule hizo.
Jedwali Namba 4: Idadi ya Shule za Sekondari kwa mwaka 2015
SHULE ZA SEKONDARI |
||||
SHULE
|
IDADI YA SHULE
|
WAVULANA |
WASICHANA |
JUMLA |
Za Serikali
|
19 |
3,287 |
3,550 |
6,837 |
Zisizo za Serikali
|
6 |
1,043 |
1,184 |
2,227 |
JUMLA KUU
|
25 |
4,330 |
4,734 |
9,064 |
IDADI YA WALIMU
Kwa mwaka 2015 Wilaya ina jumla ya walimu katika shule za sekondari za serikali 368. Kati yao 266 ni wanaume na 102 ni wanawake.
MIUNDO MBINU MUHIMU KATIKA SHULE
Hali ya uwepo wa miundombinu muhimu katika Shule za Sekondari za Serikali ni kama inavyooneshwa katika jedwali lifuatalo:-
Jedwali Namba 5: Hali ya uwepo wa Miundombinu muhimu katika Shule za Serikali – 2015
NA |
AINA YA JENGO
|
MAHITAJI
|
YALIYOPO
|
%
|
UPUNGUFU
|
%
|
1 |
Madarasa
|
200 |
175 |
87 |
25 |
13 |
2 |
Nyumba za Walimu
|
368 |
41 |
11 |
260 |
89 |
3 |
Vyoo vya Walimu (ME)
|
38 |
19 |
50 |
19 |
50 |
Vyoo vya Walimu (KE)
|
38 |
19 |
50 |
19 |
50 |
|
4 |
Vyoo vya wanafunzi (ME) matundu
|
130 |
97 |
75 |
33 |
25 |
Vyoo vya wanafunzi (kE) matundu
|
177 |
112 |
63 |
65 |
37 |
|
5 |
Majengo ya utawala
|
19 |
7 |
37 |
12 |
63 |
6 |
Maktaba
|
19 |
0 |
0 |
19 |
100 |
7 |
Bwalo
|
19 |
1 |
5 |
18 |
95 |
8 |
Hosteli za wavulana
|
38 |
1 |
3 |
37 |
97 |
Hosteli za Wasichana
|
38 |
34 |
89 |
4 |
11 |
|
9 |
Vyumba vya Maabara
|
57 |
57 |
100 |
0 |
0 |
10
|
Majiko
|
19 |
1 |
5 |
18 |
95 |
UWEPO WA VITABU SHULENI
Kimsingi, uwepo wa vitabu vya kiada katika shule za sekondari za serikali kwa masomo yote tisa ya msingi unaimarika mwaka hadi mwaka kwa namna serikali inavyoziwezesha shule kununua vitabu kupitia fedha za ruzuku (capitation grant). Hadi mwezi Februari 2015 uwiano wa kitabu kwa wanafunzi upo kati ya wastani wa 1:3 na 1:1, hasa kwa masomo ya sayansi na hisabati.
CHANGAMOTO
Sekta ya Elimu ya Sekondari katika wilaya inakabiliwa na changamoto za kimaendeleo kama ifuatavyo:-
MIKAKATI YA KUBORESHA TAALUMA KATIKA SHULE ZA SEKONDARI
CHUO CHA KILIMO CHA KARAGWE.
Wilaya na wadau wengine wa maendeleo, katika kuboresha sekta ya kilimo ambayo ndiyo uti wa mgongo wa wananchi wa Karagwe inashirikiana na dhehebu la Dini la Kilutheri Tanzania kupitia Dayosisi yake ya Karagwe lilianza ujenzi wa chuo hicho. Lengo likiwa ni kuwapata wataalamu wa kutosha wa kilimo watakaoweza kuongeza msukumo katikakuinua sekta ya kilimo Wilayani na nchi nzima kwa ujumla. Aidha chuo hiki kikikamilika kitakuwa chuo kikuu kikubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.